Kampuni ya Tanz Graphite (Tz) Limited imetoa msaada wa taulo
za kike kupitia kampeni yake ya Keep a Girl in School (Muweke msichana shuleni)
ambapo zaidi ya watoto wa kike 200 wamefaidika kwa kupata sodo za kutumia mwaka
mzima wa masomo wawapo shuleni.
Hii inatokana na changamoto kubwa inayowakumba watoto wa kike
wawapo shuleni na kwa kiasi kikubwa cha watoto wa kike huwa wanakosa uwezo wa
kusoma vyema na kuhudhuria masomo yao wawapo shuleni na kuwapelekea kukosa
vipindi. Kwa kupatiwa msaada huu watoto wa kike wanakuwa huru na uwezo mkubwa
wa kuhudhuria darasani.
Katika kampeni hii mtoto wa kike anajengewa uwezo wa kujiamini
na kujitambua na pia kuweza kujiendeleza kimaisha kwa kujengewa uwezo wa
kupambana na changamoto zinazomkabili na kuweza kuzitatua pasipo woga wowote.
Pia wanafunzi walifundishwa kuhusu usafi na matumizi bora ya sodo zenye kufaa
wakati na baada ya hedhi.
Katika tukio hili wanafunzi walifundishwa darasani ikiwemo
elimu ya idhaa ya ndoto, Dhana Binafsi na muongozo wa kazi.
Mkufunzi wa Muweke
Msichana Shuleni Ms. Camila Roshi akitoa somo kwa watoto wa shule ya sekondari
ambapo darasa hili watoto wa kike na wa kiume walijifunza elimu mbalimbali
ikiwemo Idhaa ya ndoto, dhana binafsi na muongozo wa kazi. Aliyesimama wa pili
kushoto ni mkuu wa shule ya Selina Kombani (Picha na Madam Neema)
Wanafunzi wa Shule ya
sekondari ya Selina Kombani wakipatiwa msaada wa sodo. Zaidi ya watoto 200
walipatiwa sodo za kuwatosha kwa matumizi ya mwaka mzima hasa wawapo shueni (Picha na Ms. Camila Roshi)
Wanafunzi wakifurahi
kwa kucheza ngoma za asili kwa kupatiwa msaada wa sodo kwa zaidi ya wanafunzi
200 wa kike. (Picha
na Camila Roshi)
No comments:
Post a Comment