Naitwa Olayce K Raphael nilizaliwa katika wilaya ya Arumeru katka Mkoa wa Arusha. Nilianza masomo yangu ya shule ya msingi katika shule ya olturoto primary school na kumaliza katika shule ya olkokola primary school na masomo yangu ya sekondari katika shule ya sekondari katubuka sekondari school ambapo mwalimu wangu wa mazingira mwl Asangwile Ambokile alinielekeza juu ya Roots & Shoots na ndipo nilianza juhudi za kuiomba uanachama ofisi husika na tulipewa uanachama na tulianza kutekeleza miradi katika klabu nikiwa mwenyekiti wa kamati ya wanyama na mwenyekiti wa klabu alikuwa ni Dikson Mtete mwaka 2006/2007 na mwaka 2007/2008 nilichaguliwa kuwa mweyekiti wa klabu ya katubuka sekondari abapo nilijitolea kuendesha shughuli za Roots & Shoot katika klabu yangu na nje ya klabu yangu ambapo nilianzisha kikundi cha pamoja cha Roots & Shoots wilaya ya Kigoma mjini kwa jana la NAELE group likimaanisha N-natural, A-ambassadors, of E-environment, L- life and E-education na nilikiongoza kama raisi wa kikundi hicho na pia klabu ya ngu ya Roots & Shoots ilikuwa bora kwa mwaka 2008 kwa kuweza kutekeleza miradi yake mingi na kuweza kueneza elimu ya Roots & Shoots katika wilaya ya kigoma mjini na pia niliweza kutunukiwa tuzo ya mwanachama bora katika mkoa wa kigoma kwa mwaka 2008/2009.
Pia nilipata mafunzo ya pearson foundation ya namna ya kutengeneza filamu ndani ya mwaka 2007/2008 na kuopatiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo.
Niliendelea na shughuli za kujitolea na Roots & Shoots katika mkoa wa kigoma pasipo makubaliano ya malipo yoyote na nilifanya kazi zote bila kulipwa na ofisi ya Roots and shoots na niliendelea pia katika mkoa wa Iringa kujitolea kufanya shughuli za Roots & Shoots bila malipo yoyote kutokana kwamba Roots & Shoots ilikuwa haina pesa za kuendeshea shughuli katika mikoa hiyo niliyokuwa nikifanya kazi na hapo nimejifunza namna ya kufanya kazi za Roots & Shoots katika maeneo tofauti na moyo huu wa kujitolea ni katika hali yangu ya kupenda kujifunza mambo mengi zaidi ya yale niliyojifunza na kupenda mazingira, wanyama na jamii na kutaka kujifunza mengi kuhusu Roots & Shoots. Na ninapenda nizidi kujifunza zaidi ya hapa nilipofikia nawashauri wanachama wenzangu wapende kujifunza zaidi ya kupenda maslahi kutoka katka Roots & Shoots ili tuweze kufanikiwa na kufanikisha malengo ya Jane Goodall`s Roots & Shoots duniani.
The jane goodall`s roots & shoots katika mkoa wa iringa ilianza mwaka 2009 katika shule ya sekondari kidugala seminari na mwenyekiti wa kwanza kuchaguliwa katika klabu ya kidugala ni Olayce K Raphael na katibu wake ni Eleisia Wililo na pia katika kipindi hicho cha uimarishaji wa Roots & Shoots katika mkoa wa Iringa mwenyekiti alijitahidi kuishawishi shule ili iweze kutoa kipaumbele katika klabu ya Roots & Shoots na baada ya miezi minne kupita mwenyekiti aliitambulisha rasmi klabu ya roots and shoots kwa wanaseminari wote na uongozi wa seminari kwa ujumla na klabu iliazimia kutekeleza miradi ifuatayo-;
1 kupanda maua kuzunguka maeneo yote ya shule
2 kulinda na kutoa elimu juu ya mazingira kwa ujumla.
3 kufanya budding katika miti ya miparachichi.
4 kutoa elimu ya roots & shoots kwa wanachama.
5 kutengeneza filamu inayohusu maovu ya jamii.
6 kutengeneza gazeti la klabu.
Ambapo klabu ya kidugala iliweza kutekeleza miradi yake yote iliyopangwa kutekelezwa katika mwaka 2009/2010.
Baada ya kupata uhamisho wa mwenyekiti wa klabu ya kidugala na kuweza kuhamia shule ya Mtwango sekondari Olayce K Raphael aliweza kutoa ripoti ya roots & shoots kwa uongozi wa shule ya sekondari mtwango na hapo alipewa nafasi na mkuu wa shule ya mtwango kuanzisha klabu ya roots & shoots shuleni hapo na mwalimu mlezi aliteuliwa na mkuu wa shule ambao walikuwa na mwalimu atupelye kikiva na mwalimu Joktan Mhomisoli na uongozi uliimarishwa na mwenyekiti alichaguliwa Olayce K Raphael na katibu Catherine Benedicto ambapo miradi iliyotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2010/2011 ni pamoja na-;
1 kupanda maua kuzunguka maeneo ya shule
2 kutoa elimu ya Roots & Shoots kwa wanachama wa klabu
3 kutengeneza kazi za sanaa ambazo zitaeleza matatizo mbalimbali yaliyopo katika jamii.
4 kutoa elimu ya mazingira kwa wanafunzi wote.
5 kueneza Roots & Shoots katika mazingira yanayoizunguka shule ambapo wananchi wameanzisha kikundi cha upendo group.
6 kupanda miti kuzunguka maeneo ya shule.
Katika kipindi chote cha utekelezaji wa shughuli za klabu na mkoa kwa ujumla nilikuwa nasimama kama mwakilishi wa Roots & Shoots mkoa wa Iringa nikifanya kazi chini ya makao makuu Taifa Roots & Shoots-Tanzania nikiwa na mawasiliano ya karibu na Erasto Njavike ambaye amekuwa akinipa moyo wa kupanua wigo wa Roots & Shoots na kunisaidia katika vitendea kazi vya kutolea elimu ya Roots & Shoots kwa wanachama.
Vilabu vingi vilizidi kuongezeka ambapo shule kama vile Mtwango primary school, J J Mungai sekondari Mafinga school zilituma maombi ya uanachama na nilizikubalia uanachama ambapo walitekeleza miradi yao na nilifanikiwa kufika na kutoa elimu ya Roots & Shoots ingawaje tatizo lililokuwa kubwa ni katika uchumi kwani pesa za kuweza kuendeshea shughuli za Roots & Shoots katika mkoa wa Iringa hakuna hivyo ni mpaka nipate pesa kidogo ndipo niendeshee shunguli za chama kimkoa.
Nawakaribisheni wote mtakaopenda kujifunza kuhusu roots & shoots katika shule ya mtwango sekondari na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania .
“Tutambue, tujifunze, tupange, tuelekeze na tutekeleze yale yanayohitajika katika jamii inayotuzunguka ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii zetu na taifa kwa ujumla”
Regards
Olayce K Raphael
The jane Goodall`s Roots & Shoots
Club chairperson - mtwango sec school
+255763205132
please contact naeleprogram@gmail.com for the english copy i will send to your email adress
No comments:
Post a Comment