People

Monday, September 26, 2016

KAMPUNI YA TANZ GRAPHITE WATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE (SODO) KWA WASICHANA WA SHULE YA SEKONDARI SELINA KOMBANI ILIYOPO WILAYANI MAHENGE

Kampuni ya Tanz Graphite (Tz) Limited imetoa msaada wa taulo za kike kupitia kampeni yake ya Keep a Girl in School (Muweke msichana shuleni) ambapo zaidi ya watoto wa kike 200 wamefaidika kwa kupata sodo za kutumia mwaka mzima wa masomo wawapo shuleni.
Hii inatokana na changamoto kubwa inayowakumba watoto wa kike wawapo shuleni na kwa kiasi kikubwa cha watoto wa kike huwa wanakosa uwezo wa kusoma vyema na kuhudhuria masomo yao wawapo shuleni na kuwapelekea kukosa vipindi. Kwa kupatiwa msaada huu watoto wa kike wanakuwa huru na uwezo mkubwa wa kuhudhuria darasani.
Katika kampeni hii mtoto wa kike anajengewa uwezo wa kujiamini na kujitambua na pia kuweza kujiendeleza kimaisha kwa kujengewa uwezo wa kupambana na changamoto zinazomkabili na kuweza kuzitatua pasipo woga wowote. Pia wanafunzi walifundishwa kuhusu usafi na matumizi bora ya sodo zenye kufaa wakati na baada ya hedhi.
Katika tukio hili wanafunzi walifundishwa darasani ikiwemo elimu ya idhaa ya ndoto, Dhana Binafsi na muongozo wa kazi.

Mkufunzi wa Muweke Msichana Shuleni Ms. Camila Roshi akitoa somo kwa watoto wa shule ya sekondari ambapo darasa hili watoto wa kike na wa kiume walijifunza elimu mbalimbali ikiwemo Idhaa ya ndoto, dhana binafsi na muongozo wa kazi. Aliyesimama wa pili kushoto ni mkuu wa shule ya Selina Kombani (Picha na Madam Neema)

Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Selina Kombani wakipatiwa msaada wa sodo. Zaidi ya watoto 200 walipatiwa sodo za kuwatosha kwa matumizi ya mwaka mzima hasa wawapo shueni (Picha na Ms. Camila Roshi)


Wanafunzi wakifurahi kwa kucheza ngoma za asili kwa kupatiwa msaada wa sodo kwa zaidi ya wanafunzi 200 wa kike. (Picha na Camila Roshi)